Ripoti ya Makusanyo na Matumizi ya Safari ya Kumwona Asha Rafa
Habari Wanafamilia, nipende kuchukua nafasi hii kuwashukuru kwa michango yote mliotoa kwa kuguswa na mwanafamilia mwenzetu Asha Rafa.

Team DIZASTA VINA jana tulifika mpaka nyumbani kwa Asha Rafa, Kiloleni Mwanza kumjulia hali Asha na kuifahamu familia yake, lakini pia kuwasilisha michango yetu kwake. Tulifanikiwa kuonana na yeye Asha, Mama na Kaka yake ambapo tulifanya mazungumzo tofauti ya kimaisha ili kufahamiana vyema na mazungumzo ya kimuziki, hasa muziki wa mtu aliyetuunganisha pamoja ambaye ni Dizasta Vina. Wote waliguswa na uwepo wetu pale na walifurahi sana kuona mshikamano wetu kwa ajili ya binti yetu Asha.
Mazungumzo yalitusaidia kufahamu changamoto mbalimbali ambazo Asha na familia yake wanapitia na kwa michango yetu tukawiwa kusaidia kwa kadri tulivyopata. Napenda kuwasilisha kwa muhtasari taarifa za michango na matumizi ya pesa tulizozikusanya kufanikisha safari yetu.
Michango
Tulifanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi 1,156,800 ambapo, sisi kama kikundi cha DIZASTA VINA FANS tulichangia 536,800 na kiasi kilichobakia kilitolewa na Uongozi wa Panorama (320,000) na Dizasta Vina (300,000). Kwa upekee napenda kutambua mchango wa Heri Ayoub ambaye yeye peke yake alichangia 200,000 kati ya 536,800 za wana kikundi.
Taarifa za matumizi
- Kiasi cha shilini 300,000 kilienda kulipia gharama za shule za Asha kwa ajili ya mwaka wa masomo wa 2027 zikihusisha sare za shule, michango ya chakula ambayo ni 600 kwa siku, 5000/= ya masomo ya jioni kwa mwezi.
- Kiasi cha shilingi 600,000/= kilitolewa kwa mama Asha kama mtaji wa biashara ili kuendesha familia, ikumbukwe ASHA RAFA ana ishi na wadogo zake wawili, kaka mmoja na dada mmoja. Ni mama pekee ndio mlishaji mkuu wa familia.
- Kiasi cha 265,000 kilitumika kununua mahitaji ya nyumbani ya kila siku kwa mchanganuo ufuatao
- Mchele Kilo 40 *2500 = 100,000/=
- Sukari Kilo 4 *4000=16,000/=
- Mahindi ya ugali =30,000/=
- Tambi 3 *3000= 9000/=
- Mafuta ya kula lita 5 = 28,000/=
- Madaftari 24* 1000= 24,000/=
- Counter books 12 =20,000/=
- Peni 20* 200 =4000/=
- Penseli 20*200 = 4000/=
- Dawa za meno 2 *3500=7000/=
- Sabuni michi 4*3000 =12,000/=
- Chumvi 3*1800 = 5400/=
- Usafiri wa bajaji 4000/=
- Majani ya Chai 5 *500 =2500/=
Kwa niaba ya Team Dizasta Vina na Panorama Authentik, niwashukuru wote mliojitoa kimawazo na kifedha kufanikisha tukio leo ambalo litaacha alama kwa familia ya Asha na kuongeza mshikamano baina yetu, tukiishi maono ya tungo za msanii wetu.

Kikundi kiliwakilishwa na BABA MAX ambae aliongea na ASHA RAFA pamoja na MAMA kwa simu, lakini pia DIZASTA VINA ambaye alikuwa safarini pia aliongea nao kupitia simu kuonyesha kuwa tuko pamoja.
Nawasilisha
#HipHop.

